Tanzania Airports Authority Blog

  • Home
    Home This is where you can find all the blog posts throughout the site.
Recent blog posts

Sigalla

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, Norman Sigalla, (kulia), akizungumza wakati wajumbe wa Kamati hiyo walipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere- Terminal Three (TBIII), jijini Dar es Salaam Machi 29, 2016.

George Sambali2

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, Mhandisi George Sambali, (kushoto), akitoa ufafanuzi mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, Norman Sigalla, (kulia), wakati Kamati hiyo ilipotembelea mradi wa ujenzi wa jengo la abiria la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal Three) jijini Dar es Salaam Machi 29, 2016

George Sambali2

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, Mhandisi George Sambali,(kulia), akizungumza mbele ya wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, kuhusu maendeleo ya ujenzi wa jengo la abiria la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal Three-TBIII), wakati Kamati hiyo ilipotembelea mradi huo jijini Dar es Salaam, Machi 29, 2016.

mkandarasi

Kingozi wakandarasi wa kampuni ya Uholanzi, Bam, akitoa maelezo kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya maendeleo ya Miundombinu, ikiongozwa na Mwenyekiti wake Profesa Norman Sigalla,na maafisa wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, TAA, wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Mhandisi George Sambali, wakati kamati hiyo ilipofanya ziara ya kukagua maendeleo ya mradi wa ujenzi wa jengo la abiria la uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal Three (TBIII), jijini Dar es Salaam Machi 29, 2016.

b8

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, imefanya ziara ya kutembelea mradi wa upanuzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (Terminal Three- TBIII), jijini Dar es Salaam, Machi 29, 2016 ambapo awali wajumbe wa kamati hiyo inayoongozwa na Profesa Norman Adamson Sigalla King, walipatiwa maelezo ya kina ya maendeleo ya mradi huo unaohusisha jengo la kisasa la abiria na sehemu ya kuegesha ndege kwa ajili ya kupakia na kushusha abiria na sehemu ya maegesho ya magari. Baada ya maelezo hayo ya kina yaliyotolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Nchini, (TAA), Mhandisi George Sambali akisaidiana na baadhi ya wakurugenzi wengine wa Mamlaka hiyo, wajumbe hao walitembelea mradi huo na kujionea hatua mbalimbali za ujenzi ambapo kwa sasa ujenzi umefikia karibu asilimia 60. Pichani, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali, (kushoto), akitoa maelezo kwa Mwenyekiti wa Kamati hiyo ya Bunge, Norman Adamson Sigalla King, (kulia), na baadhi ya wajumbe na maafisa wa TAA.

b6

Mwenyekiti wa Kamati, akizungumza.

b22

Kaimu Mkurugenzi wa Uwanja wa Ndege wa Julius Nyerere (JNIA), Paul Rwegasha, akizungumza na wajumbe wa Kamati hiyo ya Bunge kabla ya kutembelea mradi.

b1

Baadhi ya wajumbe wa Kamati hiyo na maafisa wa TAA, wakisikiliza maelezo yaliyokuwa yakitolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa TAA, Mhandisi George Sambali (hayupo pichani).

b2

Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga, (kulia), akitoa maelezo ya maeneleo ya mradi huo. (kushoto) ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa TAA, Laurent Mwigune.

b3

Mjumbe wa Kamati, Anna Richard Lupembe, akizungumza

b4

Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Miundombinu, na Mbunge wa Fuoni, Zanzibar, Abbas Ali Hassan Mwinyi, (kulia), akisalimiana na Mkurugenzi wa Sheria na Mahusiano wa TAA, Ramadhan Maleta, na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu, Laurent Mwigune (kushoto).

b12

Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga(kushoto), akimueleza Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Sigalla, sehemu ya maegesho ya ndege.

b14

b15

Mkurugenzi wa Mradi huo wa TBIII, Mhandisi Mohammed Millanga(kushoto), akimueleza Mwenyekiti wa Kamati, Profesa Sigalla, (kulia kwake) na baadhi ya wajumbe na maafisa wa TAA, wakiongozwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mhandisi Sambali, (wakwanza kulia), sehemu ya maegesho ya ndege.

b16

Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania, ATCL, Johnson Mfinanga akizungumzia hali ya shirika hilo.

b18

Afisa Mkuu wa Masoko wa TAA, Scholastica Mukanjanga, akizungumza.

b19

Mjumbe wa Kamati akizungumza

b20

Mjumbe wa Kamati akizungumza.

b21

Mjumbe wa Kamati, Abass Ali Hassan Mwinyi, (katikati), akizungumza.

bridge

Muonekano wa mbele (Airside) wa Ujenzi wa Jengo la tatu la abiria

Hits: 1377
0

Jengo la tatu la abiria (TB III) linalojengwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam limekamilika kwa asilimia 65.

TB III_Site_Visit_img4.jpg

Picha zaidi (Bofya)


 

Jengo hilo lenye uwezo wa kuchukua abiria milioni 6 kwa mwaka limewavutia wahandisi ujenzi kutoka mkoa wa Pwani waliolizuru leo na wadau wa usafiri wa anga jana.

Akizungumza kwa niaba ya Wahandisi wenzake leo, Mhandisi Michael Mrema amesema, mradi huo ni mkubwa, mzuri na wenye tija kwa uchumi wa nchi na kwamba wamefurahi kupata nafasi ya kujifunza ulivyo.

Meneja Mradi wa Bam International ya Uholanzi inayojenga jengo hilo, Eric Van Zuthem amesema leo, wamefurahi kupata fursa ya kuwajengea Watanzania hasa wadau wa usafiri wa anga jengo hilo la aina yake.

"Jengo hili litakuwa la kimataifa kutokana na vifaa vya usalama vitakavyofungwa hasa ukizingatia hivi sasa kuna matukio ya ugaidi kama yaliyotokea Ufaransa karibuni. Ni furaha kufanya kazi na TAA na wadau pia kuwajengea Watanzania, jengo zuri litakalovutia wageni.' amesema.

Mkurugenzi wa Mradi wa TB III, Mhandisi Mohammed Millanga amesema, mradi huo unaotekelezwa kwa awamu mbili, utakamilika mwaka 2017. Amesema awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika Juni 2016.

Amewaeleza Wahandisi hao kuwa Mkandarasi, Bam International alipewa zabuni moja ya kujenga kwa awamu mbili ambapo awamu ya pili inatarajiwa kuanza hivi karibuni baada ya Serikali kuridhia kutolewa fedha.

Amewaeleza wahandisi hao jengo hilo linajengwa kwa gharama ya Euro milioni 235 (sh. Bilioni 518). Awamu ya kwanza inagharimu Euro milioni 133.2 (sh. Bilioni 293) na ile ya pili itagharimu Euro milioni 102 (sh. Bilioni 225).

Kati ya fedha hizo, asilimia 85 inagharamiwa na Benki ya HBSC ya Uingereza kupitia mkopo unaodhaminiwa na Serikali ya Uholanzi na asilimia 15 Benki ya CRDB za mkopo unaodhaminiwa na Serikali ya Tanzania. Tayari Uholanzi imetoa fedha za awamu ya pili ili kazi ianze.

Mbali ya kuchukua abiria milioni 6, jengo hilo litakuwa na miundombinu ya madaraja makubwa ya abiria matano ya kuegesha ndege 18 na ndege moja kubwa aina ya Airbus 380. Pia litakuwa na migahawa, sehemu za kusali, watoto kucheza na theluthi moja yake ni sehemu za biashara.

Jana wadau kutoka mashirika ya ndege, wauza tiketi za ndege, wauzaji vifaa vya ujenzi, mawakala wa mizigo ikiwemo Swissport, maofisa ubalozi walizuru jengo hilo na kusifu ubora wake, miundombinu na viwango vyake.

Kutokana na abiria wanaotarajiwa kuongezeka baada ya jengo hilo kukamilika, Mhandisi Millanga amesema TAA inafikiria kuongeza njia za kurukia ndege ziwe mbili ili kukidhi mahitaji ya ongezeko la ndege zirukazo JNIA.

Amesema TAA inafikiria kuongeza njia hiyo ili moja itumiwe na ndege ndogo tu na nyingine kubwa. Kwa sasa JNIA ina njia moja ya kurukia ndege na abiria wanaopita jengo la pili la abiria, wanakadiriwa kuwa milioni 2.5.

Mwisho.

Hits: 1494
0

Contact Us

Tel (Gen): +255 22 2842402/3
Fax: +255 22 2844495
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O.Box 18000 Dar Es Salaam

Social Sites & Blog

Feedback & Enquires