Tanzania Airports Authority Blog

  • Home
    Home This is where you can find all the blog posts throughout the site.
Recent blog posts

Jengo la tatu la abiria (TB III) linalojengwa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), Jijini Dar es Salaam limekamilika kwa asilimia 65.

TB III_Site_Visit_img4.jpg

Picha zaidi (Bofya)


 

Jengo hilo lenye uwezo wa kuchukua abiria milioni 6 kwa mwaka limewavutia wahandisi ujenzi kutoka mkoa wa Pwani waliolizuru leo na wadau wa usafiri wa anga jana.

Akizungumza kwa niaba ya Wahandisi wenzake leo, Mhandisi Michael Mrema amesema, mradi huo ni mkubwa, mzuri na wenye tija kwa uchumi wa nchi na kwamba wamefurahi kupata nafasi ya kujifunza ulivyo.

Meneja Mradi wa Bam International ya Uholanzi inayojenga jengo hilo, Eric Van Zuthem amesema leo, wamefurahi kupata fursa ya kuwajengea Watanzania hasa wadau wa usafiri wa anga jengo hilo la aina yake.

"Jengo hili litakuwa la kimataifa kutokana na vifaa vya usalama vitakavyofungwa hasa ukizingatia hivi sasa kuna matukio ya ugaidi kama yaliyotokea Ufaransa karibuni. Ni furaha kufanya kazi na TAA na wadau pia kuwajengea Watanzania, jengo zuri litakalovutia wageni.' amesema.

Mkurugenzi wa Mradi wa TB III, Mhandisi Mohammed Millanga amesema, mradi huo unaotekelezwa kwa awamu mbili, utakamilika mwaka 2017. Amesema awamu ya kwanza inatarajiwa kukamilika Juni 2016.

Amewaeleza Wahandisi hao kuwa Mkandarasi, Bam International alipewa zabuni moja ya kujenga kwa awamu mbili ambapo awamu ya pili inatarajiwa kuanza hivi karibuni baada ya Serikali kuridhia kutolewa fedha.

Amewaeleza wahandisi hao jengo hilo linajengwa kwa gharama ya Euro milioni 235 (sh. Bilioni 518). Awamu ya kwanza inagharimu Euro milioni 133.2 (sh. Bilioni 293) na ile ya pili itagharimu Euro milioni 102 (sh. Bilioni 225).

Kati ya fedha hizo, asilimia 85 inagharamiwa na Benki ya HBSC ya Uingereza kupitia mkopo unaodhaminiwa na Serikali ya Uholanzi na asilimia 15 Benki ya CRDB za mkopo unaodhaminiwa na Serikali ya Tanzania. Tayari Uholanzi imetoa fedha za awamu ya pili ili kazi ianze.

Mbali ya kuchukua abiria milioni 6, jengo hilo litakuwa na miundombinu ya madaraja makubwa ya abiria matano ya kuegesha ndege 18 na ndege moja kubwa aina ya Airbus 380. Pia litakuwa na migahawa, sehemu za kusali, watoto kucheza na theluthi moja yake ni sehemu za biashara.

Jana wadau kutoka mashirika ya ndege, wauza tiketi za ndege, wauzaji vifaa vya ujenzi, mawakala wa mizigo ikiwemo Swissport, maofisa ubalozi walizuru jengo hilo na kusifu ubora wake, miundombinu na viwango vyake.

Kutokana na abiria wanaotarajiwa kuongezeka baada ya jengo hilo kukamilika, Mhandisi Millanga amesema TAA inafikiria kuongeza njia za kurukia ndege ziwe mbili ili kukidhi mahitaji ya ongezeko la ndege zirukazo JNIA.

Amesema TAA inafikiria kuongeza njia hiyo ili moja itumiwe na ndege ndogo tu na nyingine kubwa. Kwa sasa JNIA ina njia moja ya kurukia ndege na abiria wanaopita jengo la pili la abiria, wanakadiriwa kuwa milioni 2.5.

Mwisho.

Hits: 1690
0

BANDA la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) limekuwa kivutio kikubwa kwenye maonesho ya 22 ya Nanenane kutokana na wananchi wengi kufurika ili kupata ufafanuzi na maelezo yanayohusu viwanja vya ndege nchini. Maonesho hayo yenye kaulimbiu "Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji", yanaendelea kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi yakishirikisha Wizara mbalimbali na Taasisi zake. Maonesho ya kwanza ya kilimo yalifanyika mwaka 1993 katika Uwanja wa Uyole Jijini Mbeya.

Wakinamama wakipata maelezo ya shughuli za Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) kutoka kwa Meneja wa kiwanja cha ndege wa Lindi, Margareth (aliyekaa kulia).

 Wakazi wa Lindi waliotembelea banda la Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) wakipiga picha ya pamoja na wafanyakazi wa TAA.

 

 Wananchi wakitazama picha za 'video' zenye kuonyesha zoezi la uokoaji lililofanyika kwenye Kiwanja cha Ndege cha Julius Nyerere (JNIA).

 Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akipata maelezo kwenye banda la Bima ya Afya wakati akitembelea maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Mh. Halima Dendego.

 Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akipata maelezo kwenye banda la Bima ya Afya wakati akitembelea maonesho ya sikukuu ya wakulima Nanenane yanayoendelea mkoani Lindi. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Mwantumu Mahiza.

 Waziri Mkuu, Mhe. Mizengo Pinda akiwahutubia wananchi wa Lindi na Mtwara katika uzinduzi wa maonesho ya 22 ya sikukuu ya wakulima, yanayofanyika kitaifa mkoani Lindi.

 

Wafanyakazi wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TAA) Walioshiriki Maonesho ya Nane Nane 2015 Mkoani Lindi

Hits: 1987
0

Contact Us

Tel (Gen): +255 22 2842402/3
Fax: +255 22 2844495
Email: This email address is being protected from spambots. You need JavaScript enabled to view it.
P.O.Box 18000 Dar Es Salaam

Social Sites & Blog

Feedback & Enquires